Luke 9:1-2

Isa Awatuma Wale Kumi Na Wawili

(Mathayo 10:5-15; Marko 6:7-13)

1 aIsa kisha akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa mamlaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote, 2 bkisha akawatuma waende wakahubiri Ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.
Copyright information for SwhKC